Huyu kocha mpya wa Yanga Pedro Goncalves amehudumu kama Mng’amuzi wa Vipaji, katika Klabu ya Sporting CP kabla ya kujiunga na Kituo cha kulelea vipaji cha Sporting CP kati ya mwaka 2000 hadi 2015.
Kwa aina ya vijana waliopo Yanga kwa sasa wanaweza kukutana na urahisi wa kucheza kama wataonyesha uwezo wao hapa nawazungumzia kina Casemiro, Ninju , Nkane na wenzie
Kwa mara ya kwanza Barani Afrika alifika mwaka 2015, akiifundisha timu ya vijana ya Premeiro de Agosto, alihudumu hadi 2018.
Mradi wa maendeleo ya soka la Angola ulioanzishwa na Chama cha Soka Angola mwaka 2018 ulimfanya Pedro Goncalves akabidhiwe mradi wa vijana chini ya miaka 17.
Aliifundisha timu hiyo pamoja na ile ya vijana chini ya miaka 20 hadi 2019 na kukabidhiwa timu ya Angola ya Wakubwa.
Angola aliifundisha kuanzia 2019 hadi 2025 alipofukuzwa. Pedro, aliiongoza Angola kwenye mashindano ya CHAN. Mradi wa sasa wa Angola umesukwa chini yake na ndiye aliyeusimamia tangu 2018.
Mchezo wake kwa kwanza Pedro ni kesho kutwa ligi kuu






