Tottenham Hotspur wamemfanya winga wa Everton, Iliman Ndiaye, 25, kuwa mchezaji anayelengwa zaidi, lakini Newcastle United, Juventus, AC Milan na Atletico Madrid pia wanamfuatilia mchezaji huyo. (TeamTalk)
Chelsea na Tottenham wanafikiria uhamisho wa Januari kwa mshambuliaji wa Juventus na Canada Jonathan David, 25 (TuttoMercatoWeb)
Everton inaweza kuhamia kwa mshambuliaji wa Midtjylland, Franculino Dju, 21, mwezi Januari lakini inakabiliwa na ushindani kutoka Bologna kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Guinea-Bissau. (Sun)
Liverpool wako tayari kutoa euro milioni 100 (£88m) kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Italia Alessandro Bastoni, 26, kutoka Inter. (Il Giorno)
Real Madrid watakuwa tayari kutumia euro milioni 250 (£220m) kwa kiungo wa Arsenal na Uingereza Declan Rice, 26, na winga wa Ufaransa wa Paris St-Germain Bradley Barcola, 23. (Fichajes)
Barcelona wanavutiwa na beki wa Crystal Palace na Colombia Daniel Munoz, 29. (Mundo Deportivo)
Mshambuliaji wa Levante Etta Eyong, 22, anafuatiliwa na Real Madrid na Barcelona, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon anasema itakuwa “ndoto” siku moja kuichezea Chelsea katika Ligi Kuu. (Givemesport)
Meneja wa Manchester United Ruben Amorim anaweza kutafuta kuimarisha safu yake ya ushambuliaji mwezi Januari ikiwa jeraha la goti la mshambuliaji wa Slovenia Benjamin Sesko mwenye umri wa miaka 22 litakuwa kubwa, kwani tayari anakabiliwa na kupoteza mshambuliaji wa Cameroon Bryan Mbeumo, mwenye umri wa miaka 26, na Amad Diallo wa Ivory Coast, mwenye umri wa miaka 23, wakiwa katika majukumu ya kimataifa katika Kombe la Mataifa ya Afrika. (Mirror)







