Mshambuliaji matata wa Simba SC, Steven Mukwala, anadaiwa kuwa mbioni kutua Raja Casablanca ya Morocco katika dirisha dogo la usajili. Inaelezwa kuwa kocha wa Raja, Fadlu Davids, ambaye aliwahi kumfundisha Simba, ndiye anayepanga “kumpora” nyota huyo kutoka Msimbazi.
Vyanzo vya karibu na klabu vinaeleza kuwa Simba wako tayari kumuachia Mukwala kutokana na uwepo wa washambuliaji wengine kama Jonathan Sowah na Seleman Mwalimu, huku uongozi ukipanga kufanya “maboresho makali” kwenye safu ya ushambuliaji.
Inaelezwa pia kuwa Mukwala kwa sasa hana furaha kama awali ndani ya klabu, jambo linalozidisha uvumi wa kutaka kutafuta changamoto mpya nje ya Tanzania.
The post Mshambuliaji wa Simba Steven Mukwala Kutimkia Raja Casablanca appeared first on SOKA TANZANIA.





