NYON: Mashabiki wa klabu ya soka ya Young Boys wamezuiwa kuhudhuria mchezo wa Europa League wa alhamisi Alhamisi ijayo kama adhabu kwa vurugu zao zilizokatisha mchezo dhidi ya Aston Villa wiki iliyopita.
Mashabiki wa Young Boys walirusha chupa za plastiki zilizompiga mfungaji wa Aston Villa, Donyell Malen, na kugombana na walinzi wa uwanjani walipopokea kichapo cha mabao 2-1 mchezo wa Novemba 27 mwaka huu. Mchezo uliosimamishwa kwa takribani dakika tano katika kipindi cha kwanza.

UEFA imesema Pamoja na adhabu hiyo jopo lake la nidhamu pia limeipiga Young Boys faini ya euro 50,000 na kuipiga marufuku klabu hiyo kuuza tiketi kwa mashabiki wake kwa mchezo ujao wa ugenini wa Europa League.
Young Boys watacheza ugenini dhidi ya Stuttgart Januari 29 katika mzunguko wa mwisho wa hatua ya ligi ya michuano hiyo.
The post UEFA yawafungia mashabiki wa Young Boys first appeared on SpotiLEO.






