Mshambuliaji wa zamani wa klabu za TP Mazembe, AS Vita Club na Yanga SC, Chico Ushindi Wakubanza, amefariki dunia leo mchana akiwa nyumbani kwao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Chico Wakubanza alikuwa mmoja wa washambuliaji waliopata heshima kubwa katika soka la Afrika na Kati na Mashariki, akitambulika kwa uwezo wake wa kufumania nyavu, nguvu ya kimwili na uzoefu mkubwa katika ligi mbalimbali. Enzi zake akiwa uwanjani zilimpa jina la “Striker la Mabao”, akiacha alama isiyofutika kwa mashabiki na vilabu alivyovitumikia.
Kifo chake ni pigo kubwa kwa familia, marafiki, jumuiya ya soka barani Afrika na mashabiki wa Yanga, TP Mazembe na AS Vita Club.
Pumzika kwa Amani ‘Striker’ la Mabao, Chico Wakubanza Ushindi







