Na Said Mwishehe,Michuzi TV
JUZI
kati nilikuwa na mshikaji wangu fulani hivi basi tukawa tunapiga stori
kuhusu nchi yetu chini ya uongozi wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan
Katika
mazungumzo yetu tukakubaliana kwa kauli moja Rais Dk.Samia tunampenda
na katika uchaguzi mwaka huu tutamchagua tena kiroho safi.Tunampenda
naye anatupenda.
Zipo sababu nyingi za kumchagua Rais Samia katika uchaguzi mkuu mwaka 2025.Ukweli hatuna shaka naye na kwa sasa tunatamba naye.
Kabla
ya kueleza baadhi ya sababu ambazo zinanifanya mimi na Watanzania
wenzangu kumchagua Rais Samia katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 nitumie
pia nafasi hii kuipongeza CCM kupitia Mkutano Mkuu maalum uliofanyika
Januari 18 na 19 mwaka huu kupitisha azimio.
Katika azimio hilo
limeweka wazi kuwa mgombea wao wa nafasi ya urais kwa tiketi ya Chama
hicho ni Rais Dk.Samia Suluhu Hassan na Mgombea Mwenza ni Dk.Emmanuel
Nchimbi ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa Chama hicho.
Hongereni
CCM kwani azimio lenu ndio azimio letu, mawazo yenu ndio mawazo
yetu,matarajio yenu ndio matarajio yetu.Yaani kwa lugha ya mjini
tunasema 2025 Samia mitano tena,ndio eeeeh kama inakuuma sema.
Kwa
jinsi ambavyo Rais Samia anaongoza nchi yetu tunaona kabisa nchi
imetulia, iko tulivu na hakuna anayeishi kwa hofu,tunajivunua uongozi wa
Rais Samia.
Wakati anakabidhiwa Nchi wapo waliodhani hataweza,
hatafanya lolote hata miradi ya kimkakati haitakamilika lakini hivi sasa
sote ni mashahidi Rais Samia ameweza na mambo yanakwenda, tunaraha
wenyewe,hongera Rais Samia,tunakupenda na tutakuchagua.
Chini ya
uongozi wa Rais Dk.Samia watanzania tunashuhudia utekelezaji wa miradi
ya kimkakati iliyopo katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu,mambo ni
moto,mambo ni faya.Miradi mingi imekamilika na mingine iko hatua za
mwishoni.
Reli ya SGR leo ni mwendo wa kuteleza tu, unalala Dar
na chai unakunywa Dodoma. Ukiondoka saa 12 kamili asubuhi Dar basi
Dodoma utafika kwenye saa 3:42 au 3:45 kama hakutakuwa na changamoto.
Chini
ya Rais Samia amehakikisha SGR ujenzi wake unaendelea na ujenzi wa reli
hiyo umefika Makutupola na kazi inaendelea kuelekea Mwanza,Tabora
pamoja na Kigoma.Mama Samia yupo kazini kwa kifupi kazi inaendelea.
Katika
mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere kule Rufiji mitambo imewashwa na
Watanzania tumeanza kujibweda,mgao wa umeme umekwisha na kama kunakuwa
na mgao basi ni ule unaotokana na uchakavu wa miundombinu ambayo nayo
uboreshaji wake unaendelea.Hongera Rais Samia tunakupenda na
tutakuchagua.
Ujenzi daraja la Kigongo-Busisi katika Ziwa
Victoria mambo safi , kazi ya ujenzi iko mwishoni na muda si mrefu
tutashuhudia magari yakipita.Kwa wanaofuatilia wanajua wakati Rais Samia
anaingia madarakani ujenzi ulikuwa umefikia hatua gani?Wakati Rais
Samia anachukua Nchi daraja hilo ndio kwanza nguzo zilikuwa zimeaanza
kuwekwa lakini leo hii ujenzi zaidi ya asilimia 95.
Kwa ambaye
haamini ninachoeleza basi anayo nafasi ya kufunga safari aende kuangalia
maana wengine wako kama Tomaso hawaamini mpaka waone.
Kwa kazi
ambayo Rais Samia hakika tutalipa fadhila na shukrani zetu katika boksi
la kura.Ametuheshimisha Watanzania na sisi tutamheshimisha kwa kumpigia
kura.
Nafahamu kura ni siri ya mpigakura lakini kwa Samia wala
hakuna siri kura yangu ni ya kwake na kura za Watanzania zote ni kwa
Samia.
Kwa aliyofanya Samia kazi yetu ni kumpigania,kumtetea na
kumuombea afya na uzima .Ikifika siku ya kupiga kura basi tukampigie
kura.
Wakati natafakari yaliyofanywa na Rais Samia nimekumbuka
jinsi ambavyo amefanikiwa kutibu ugonjwa wa miaka mingi wa uhaba wa
madarasa hasa kwa shule za sekondari.
Kwa miaka mingi ilikuwa
kila mwaka lazima wanafunzi wanaokwenda kidato cha kwanza wasubirie
ujenzi wa madarasa ndio waende sekondari.Wakurugenzi na wakuu wa mikoa
walikuwa wananyimwa likizo kisa wasimamie ujenzi.
Chini ya Rais
Dk.Samia wanafunzi wote wanaotakiwa kujiunga na elimu ya sekondari
wanaanza masomo siku moja kwa tarehe husika ambayo shule
itafunguliwa.Katika hili Rais Samia anastahili pongezi.
Kwa
upande wa huduma za maji Rais Samia kupitia Serikali anayoiongoza
imeendelea kutatua changamoto ya uhaba wa maji safi na salama.Kupitia
RUWASA ambao wanahusika na kusambaza maji vijijini wanaendelea na kazi
ya kusambaza maji.
Kuna vijiji ambavyo tangu nchi ipate huru
havikuwahi kupata maji safi na salama katika bomba lakini chini ya Rais
Samia leo wananchi wanapata maji.Tunaposema Rais Samia tunampenda
kwasababu yeye mwenyewe anaupendo mkubwa kwetu.
Rais Samia tangu ameingia madarakani ameendelea kutafuta ufumbuzi wa changamoto hatua kwa hatua na hili tunajivunia Watanzania.
Huduma za afya zimeendelea kuboreshwa na sasa dawa na vifaa tiba vya kisasa viko kuanzia zahati mpaka hospitali za rufaa.
Katika
miundombinu ya barabara tunaendelea kushuhudia kazi inayofanywa na Rais
Samia.Barabara zinaendelea kujengwa kila mahali na kwa Dar ea Salaam
ujenzi barabara ya mwendo kasi kazi inaendelea na wakandarasi wako
saiti.
Kauli mbiu ya Rais Samia inasema Kazi iendelee na kweli
kazi inaendelea.Kama huamini kawaulize wa kulima.Ujenzi wa miundombinu
ya umwagiliaji unaendelea kila mahali,Rais ametoa mabilioni ya fedha
kutekelezwa kwa miradi.
Hapo sijazungumzia upatikanaji wa pembejeo za kilimo.Hakuna yale malalamiko mbegu imechelewa,mbolea haijafika.
Kwa
kazi ambayo Rais wetu Dk.Samia ameendelea kuifanya na kuonekana zawadi
pekee ambayo anastahili kupewa ni kushinda kwa kishindo.Sina mashaka
hata kidogo ushindi ni kwa Dk.Samia
Lakini tuwe wa kweli katika
uongozi wa Rais Samia ameendelea kusimamia haki za watu, uhuru wa
kujieleza na kutoa maoni.Rais Samia ameponyesha majeraha kwa baadhi ya
watu.Vilio vimepungua kikubwa kila mmoja afanye shughuli zake kwa mujibu
wa utaratibu uliowekwa.
Utulivu katika shughuli mbalimbali
zikiwemo za kiuchumi zimesababisha hata mapato ya kodi kupaa.Nchi iko
vizuri katika makusanyo ya kodi na Rais anasisitiza watu kuendelea
kulipa kodi kwa inavyostahili.Asidhulumiwe mwananchi, wala Serikali
isidhurumiwe.
Kabla ya kuhitimisha nimekumbuka dhamira njema ya
Rais Samia katika kuboresha bandari zetu ikiwemo ya Dar es Salaam ambapo
kuna baadhi ya watu walipinga uwekezaji wa DP World.Leo hii bandari ya
Dar es Salaam hakuna tena msongamano wa meli bandarini, meli inakuja
inashusha kontena na kuondoka.
Tafsiri kubwa katika uwekezaji wa
bandari Rais Samia aliona mbali,alitazama maslahi mapana ya Nchi yake na
leo tumeanza kuvuna matunda ya uwekezaji uliofanyika.Hongera Rais
Samia,tunakupenda,tutakuchagua .Yaani mitano tena kwako Rais wetu.