Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah
Hassan Mitawi akifungua Kikao cha Maandalizi ya Ligi ya Muungano kuelekea
Maadhimisho ya Miaka 61 ya Muungano kilichofanyika jijini Dar es Salaam Februari 18, 2025.
Mkurugenzi wa Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Juma Mohamed
Salum akiongoza Kikao cha Maandalizi ya Ligi ya Muungano kuelekea
Maadhimisho ya Miaka 61 ya Muungano kilichofanyika jijini Dar es Salaam
Februari 18, 2025. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Muungano Bi. Hanifa Selengu.
Sehemu ya washiriki wakifuatilia Kikao cha Maandalizi ya Ligi ya Muungano
kuelekea Maadhimisho ya Miaka 61 ya Muungano kilichofanyika jijini Dar es
Salaam Februari 18, 2025. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Muungano Bi. Hanifa Selengu.
…………
Serikali imetoa wito kwa Vyama vya Michezo vya Tanzania Bara na Zanzibar
kushirikiana na kubadilishana uzoefu ili kuendeleza mshikamano baina ya
wananchi wa pande zote mbili na kudumisha Muungano.
Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa
Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi akifungua Kikao cha Maandalizi ya Ligi ya
Muungano kuelekea Maadhimisho ya Miaka 61 ya Muungano kilichofanyika
jijini Dar es Salaam Februari 18, 2025.
Lengo la kikao hich ni kufuatilia na kuweka mkakati wa kutekeleza agizo la
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
wakati wa Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano mwaka 2024 kuhusu
kurejeshwa kwa Ligi ya Muungano kwa lengo la kudumisha Muungano.
Akizungumza na wadau wa michezo kutoka vyama mbalimbali nchini, Naibu
Katibu Mitawi amesema Wizara zinazosimamia Michezo zina wajibu wa
kuhahakima azma ya Mheshimiwa Rais inatimizwa.
“Ndugu zangu, tunatambua kwamba michezo ilikuwa ni kielelezo cha
mshikamano kwa watu kukutana na kutumia nafasi hiyo kupenyeza agenda
zingine, hususani wakati wa kudai Uhuru,“ ameeleza.
Aidha, Naibu Katibu Mkuu Mitawi ameongeza kuwa Wizara zinazosimamia
sekta ya michezo Tanzania Bara na Zanzibar zina wajibu wa kuhakikisha azma
ya Mhe. Rais Dkt. Samia inatimizwa.
Hivyo, Naibu Waziri Mkuu ametumia wasaa huo kuwasihi washiriki wa kika
hicho kujadili kwa uzito na kutoka na maazimio ya namna bora katika
kutekeleza agizo hilo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt.
Juma Mohamed Salum amesema lengo la kukutana wadau hao na Serikali ni
kujadili na kufikia hatua nzuri kuyafanya mashindano ya Muungano kuwa
endelevu.