Mwenyekiti
wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Kuombea uchaguzi mkuu 2025 ndugu
Alex Msama, anatarajia kufanya tamasha kubwa la kuombea uchaguzi nchi
nzima,akianza na jiji la Dar es Salaam.
wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Kuombea uchaguzi mkuu 2025 ndugu
Alex Msama, anatarajia kufanya tamasha kubwa la kuombea uchaguzi nchi
nzima,akianza na jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam,Mwandaaji wa tamasha
hilo Ndugu Alex Msama, amesema tamasha hilo linatarajiwa kufanyika mwezi
wa 4 kwa tarehe rasmi itakayopangwa katika jiji la Dar es Salaam na
baadae litasambaa katika mikoa mingine 26 ya Tanzania Bara.
“kwa
ujumla Maandalizi ya tamasha hilo mpaka sasa yanaendelea vizuri,na
tunawakaribisha Wadhamini mbalimbali kuja kutuunga mkono kufanikisha
Tamasha hili kubwa ambalo maalum kuomba uchaguzi ufanyika kwa
amani,upendo na utulivu”,amefafanua Ndugu Msama .
Amesema
kwa sasa jambo kubwa linalofanyika ni kuendelea kuzungumza na wafadhili
mbalimbali, na kwamba wakifanikiwa kupata Wadhamini, basi tamasha hilo
litakuwa halina kingilio,Watu wote wataingia bule.
Akifafanua
zaidi Msama amebainisha kuwa tamasha hilo lenye umuhimu mkubwa kwa nchi
yetu,hasa kwa wakati huu tunaokwenda kwenye uchaguzi,litawakutanisha
waimbaji mbalimbali wa nyimbo za injili ndani na nje ya nchi.