Naibu Katibu Mkuu wa Taasisi ya Twarika Taifa ,Shehe Haruna Hussein akizungumza katika hafla hiyo ya futari jijini Arusha

Waumini wa dini hiyo wakifuturu baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutoa fedha kwa ajili ya kufuturisha waumini hao .



Happy Lazaro,Arusha .
WAUMINI wa Taasisi ya dini ya kiislamu ya Twarika Zawiya Kuu mkoani Arusha wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia fedha zitakazotumika kufuturisha futari katika kipindi cha mfungo wa Ramadhani .
Akizungumza katika futari hiyo kwa waumini hao mkoani Arusha ,Naibu Katibu Mkuu wa Taasisi ya Twarika Taifa ,Shehe Haruna Hussein amesema kuwa ,anamshukuru sana Rais Samia kwa namna ambavyo ameonyesha moyo wa kipekee katika kutoa futari kwa waumini hao na kuweza kutambua uwepo wao.
Shehe Haruna akizungumza katika futari hiyo amewataka waumini hao wa dini ya kiislamu kujenga tabia ya umoja na ushirikiano na kuacha kiburi badala yake wawe na hofu ya Mungu .
“Yeyote atakayeenda kinyume na sisi kama viongozi wa mkoa hatutamwacha tutakuwa sambamba na kukemea tabia hiyo mara moja tunataka kuona viongozi wakisikilizwa .”amesema Shehe Haruna .
“Waislamu sasa hivi tuache kusemana kama mtu amekosea muite pembeni umweleze alichokosea na sio kwenda kukaa pembeni na kuacha kumsema ,tunaenda na viongozi wanaojitambua na kuwajibika.’amesema.
Shehe Haruna amesema kuwa, hapendi kukaa kama mzigo kwenye Taasisi bali anataka kufanya kazi huku akihakikisha waislamu wote wanakuwa kitu kimoja na lengo moja.
Kwa upande wake mgenirasmi katika futari hiyo Shehe Hamis Migire amemshukuru Rais Samia kwa namna ambavyo ameonyesha moyo wa kipekee na kuwakumbuka katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani .
Amewataka viongozi wa Taasisi hiyo wakawe viongozi wajasiri ambao hawaogopi maneno ya watu kwani mtu yeyote akiwa kiongozi akisemwa anapandishwa daraja hivyo amewataka wawe wavumilifu,subira na kupendana .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Taifa ,Shehe Mubarak Salim amesema kuwa,kitendo kilichofanywa na Rais Samia ni kikubwa sana hivyo wamemshukuru sana kama viongozi huku wakiahidi kuwa pamoja naye katika kutoa ushirikiano wa pamoja na serikali .