Na. Mwandishi Jeshi la Polisi Arusha.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema kuwa linapenda kutoa ufafanuzi juu ya taarifa inayosambaa katika Mitaandao na picha mjongeo ikimwonesha mwananchi mmoja aitwae Mercy Daniel Mkazi wa Arusha ambaye ameeleza kupotea kwa mmewake aitwae David Gipson Mkazi wa Arusha huku likiweka Wazi kuwa Mtu huyo ashirikiwi na Jeshi hilo.
Akitoa taarifa hiyo leo Machi 18,2025 kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Justine Masejo amesema kuwa Jeshi hilo limepokea taarifa hiyo na uchunguzi wa shauri hilo unaendelea, katika ufuatiliji huku akibainisha kuwa uchunguzi wa awali ukibaini kuwa David Gipson amehusishwa na upotevu wa fedha uliotokea katika benki moja hapa jijini Arusha jina akisema jina wanalihifadhi.
SACP Masejo ameongeza kuwa Jeshi la Polisi Mkoani humo linaendelea na ufuatiliaji wa shauri hilo ili kubaini mtu huyo yuko wapi na taarifa kamili itatolewa.
Akatoa wito kwa wananchi kusaidia Jeshi la Polisi kutoa taarifa za mtu huyo popote atakapoonekana. Pia kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili Mkoa wetu uendelee kuwa shwari.