Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimeibuka mshindi wa Pili katika Tuzo za Afya na Usafi wa Mazingira kwa kundi la Vyuo Vikuu Tanzania Bara.
Tuzo hii imetolewa na Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama (Mb), akimuwakilisha Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika hafla iliyofanyika Jumanne, tarehe 8 Aprili, 2025, kwenye ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Mashindano haya yaliyoandaliwa na Wizara ya Afya ikiwa ni kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Afya Kitaifa Mwaka 2025. Ushindi huu unaonesha jitihada kubwa zinazofanywa na SUA katika kuweka mazingira safi na salama kwa wanafunzi, wafanyakazi, na jamii inayozunguka Chuo.
Ushindi huu unatarajiwa kuongeza chachu kwa SUA kuendelea kuboresha zaidi masuala ya afya na usafi wa mazingira na kuhamasisha Wanajumuiya wake kuendelea kuboresha usafi wa mazingira.
Maadhimisho hayo yaliyoongozwa na kauli mbiu isemayo Tulipotoka, Tulipo, Tunapoelekea; Tunajenga Taifa Lenye Afya.