Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi amewataka wakandarasi wasiokuwa na uwezo wa kufanya kazi kuacha kuomba kazi Mkoani mara kwani Mkoa huo siwamajaribio.
Kanali Mtambi ametoa kauli hiyo Akiwa wilayani Tarime Mkoani mara baada ya kutembelea ujenzi wa shule mpya ya sekondari Kibumaye iliyoko wilayani humo ambapo amesema hajaridhishwa na Kasi ya utekelezaji wa Miradi nakuwataka wakandarasi kuacha kuufanya mkoa wa Mara kuwa Mkoa wa majaribio ya utekelezaji wa Miradi.
Mtambi amesema sikwa wakandarasi pamoja wa watu wengine wanaomba tenda mbalimbali ikiwemo za usambazaji wa vifaa yaani wazabuni nao kujiepusha na Rungu litakalopitishwa kwao.
“Wakandarasi kama unaona huna uwezo usiombe Mradi katika Mkoa huu wa mara hatutaki majaribio kwenye Mkoa huu tunataka watu walioko tayari kufanya kazi”Alisema kanali Evans Mtambi Mkuu wa Mkoa wa Mara.