Na Silivia Amandius.
Kyerwa, Kagera.
Wananchi katika halmashauri ya wilaya ya kyerwa wameishukuru serikali ya jamuhuri ya muungano ya Tanzania kwa kuleta kampeini ya msaada wa kisheria ya Mama samia kwani imemulika migogoro ya ndoa ambayo upelekea kuwa chanzo cha migogoro ya Ardhi.
wakizungumza baadhi ya wananchi wa kata mabira kijiji cha kibimba na mabira katika mkutano wa adhara akiwemo Bw. Philibat France na Mathayo Bernard wemesema kuwa kuwepo kwa ujio wa kampeini hii katika ngazi ya vijijini inaenda kuwa mkombozi kwani familia nyingi zipo katika hali mbaya.
Aidha wameongeza kuwa familia nyingi zimekuwa na changamoto ya migogoro ya ndoa inayosababishwa na watoto wao wenyewe ambayo mwisho wa siku inasababisha migogoro ya ardhi mpaka kupelekea kufanyiana vitendo vibaya wakati mwingine kwani asilimia kubwa ya waathirika katika mgogoro hiyo ni wanaume hasa pale wanapopigwa na wakezao wenyewe.
Pia wamesema kupitia uelewa walioupata kutoka kwa Wataalamu hao itasaidia kukuza malezi bora ya familia zao hasa kwa watoto na kuwa na uelewa juu ya mirathi katika familia zao.
Nae bi Getruda Mwiga kutoka dawati la jinsia na watoto ambae nae ni miongoni mwa timu ya msaada wa kisheria ya mama samia amewasihi wazazi kudumisha malezi bora kwa watoto wao kwani hiyo itasaidia kuondoa changamoto hizo katika jamii.
“Malezi bora kwa watoto wetu ni muhimu ila pia kama familia tunatakiwa kusikiliza na pia unapopata changamoto usisite kutoa taarifa ili kupata msaada mfano kwa wakina baba najua mnakutana na changamoto nyingi huko katika makazi yenu ila msiwe na aibu kutoa taarifa kwani itawasaidia kutojichikulia sheria mkononi”
Kwa upande wake afisa ardhi mwandamizi Bw. Bitabonwa Mkama amesema kila mwananchi anayo haki ya kumiliki ardhi kisheria bila kubagua jinsia na kupitia kampeini hii ya msaada wa kisheria itakuwa ni fursa kupata msaada wa kisheria.
Sambamba na hayo pia bw. Bitabonwa katika kutoa elimu hiyo ya msaada wa kisheria juu ya umiliki wa ardhi amekutana na changamoto ya kutokuwepo kwa mabaraza ya ardhi ya vijiji jambo linalopelekea migogo mingi ya ardhi katika vijiji hivyo ambapo amehaidi kufanyiwa kazi kupitia kampeini hiyo.