Na Prisca Libaga Arusha
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini Aprili 11, 2025 imetoa elimu juu ya madhara ya tatizo la dawa za kulevya kwa umma katika Mkutano wa Kiinjili wa Kanisa la Kisabato katika Eneo la Soko la Kilombero jijini Arusha.
Aidha, washiriki wa Mkutano huo zaidi ya 120 walielezewa jinsi malezi duni yanavyoweza kusababisha watoto na vijana kuingia katika matumizi au biashara haramu ya dawa za kulevya.
Pia, washiriki hao walikumbushiwa wajibu wao wa kuendelea kushirikiana na Mamlaka kwa kutoa taarifa za wahalifu wa dawa za kulevya kwa kupiga namba ya simu ya bure ya 119.
Ofisi ya Mamlaka Kanda ya Kaskazini itaendelea kushirikiana ma Viongozi wa Dini zote kuhakikisha waumini wao katika nyumba za ibada wanafikiwa na elimu juu ya madhara ya tatizo la dawa za kulevya.


