Wakati Serikali ikiwekeza Nguvu kubwa katika Michezo mbalimbali hapa Chini wadau Mkoani Mara wameombwa kushirikiana kuiunga Mkono jitihada hizo katika utengenezaji wa viwanja pamoja na ununuzi wa vifaa vya Michezo mashuleni.
Kauli hiyo imetolewa na Mdau wa Michezo Dk Wilson Mkama Wakati wa kuahirisha mashindo ya Umitashmta yaliyofanyika Wilayani Tarime Mkoani mara katika Nchini wa Kupata wanamichezo 120 watakaoelekea katika Mkoani Iringa katika mashindano ya Kitaifa.
Mkama amesema kama wadau wanayofursa na nguvu ya KUWEKEZA katika viwanja vya Michezo ili kusaidia kuibua vipaji pamoja na kutengeneza Kesho ya vijana wenye ndoto katika michezo.
Katika hatua nyingine DK Wilson Mkama ameahid kutoa kiasi cha fedha ambacho kitasaidia maandalizi ya Mashindano ya Umitashmta kwa shule za Msingi pamoja na kutoa jezi katika maandalizi ya yajayo ili kutengeneza motisha kwa Vijana.