Mwanasheria wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT), Vick Mbunde, akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Nyumbu wakati akitoa elimu ya sheria ya makosa ya kimtandao Kibaha Mkoa wa Pwani Aprili 24, 2025.
Na Mwandishi Wetu, Kibaha
TUME ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT), imeto elimu kwa wananchi zaidi ya Milioni 2 katika mkoa wa Pwani, Lindi na
Mtwara inayohusu Sheria ya makosa ya kimtandao, maadili na ulinzi wa mtoto
dhidi ya makosa hayo.
Mwanasheria wa Tume hiyo, Vicky Mbunde, akizungumza kwa nyakati tofauti Kibaha mkoani Pwani Aprili 24, 2025
wakati akitoa elimu kwa wanafunzi wa Chuo cha Walimu cha A3, Uuguzi na Uandishi
wa Habari pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Nyumbu aliwataka kuwa
mabalozi na walinzi wa mtoto dhidi ya makosa ya kimtandao huku wakijiepusha
kufanya makosa hayo.
Alisema makosa ya kimtandao yamekuwa
yakitumika kwa kutumia vifaa vya kielektroniki kama kompyuta, simu janja na
vishikwambi na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
“Makosa hayo ni kurekodi picha mbaya
za watoto kama za utupu, kufanyiwa vitendo vya ukatili, kudhalilishwa na
vitendo vingine vinavyofanana na hivyo na kuzisambaza mtandaoni,” alisema
Mbunde.
Mbunde alisema mwanafunzi yeyote
atakapoona vitendo hivyo vikifanyika au anafanyiwa atoe taarifa kwa walimu,
wazazi na polisi ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
Alisema vitendo hivyo havikubaliki
katika jamii na ndio maana zimetungwa sheria kali dhidi ya mtu yeyote
atakayebainika kutenda makosa hayo.
Wakili Baraka Chipamba kutoka tume
hiyo alisema makosa yote hayo yakiwepo ya ubakaji, kutia mimba na utoaji wa
mimba adhabu yake ni kifungo cha zaidi ya miaka mitano nafaini kuanzia shilingi
milioni tano hadi milioni 20 au zote kwa pamoja.
Walimu wa shule hizo waliipongeza
tume hiyo kwakutoa elimu hiyo na wakaomba iwe endelevu kwani itasaidia
kuwaondolea watoto hao madhira ambayo yanaweza kuyapata kutokana na vitendo hivyo.
Tume hiyo inatoa elimu hiyo chini ya
Kaulimbiu isemayo Mabadiliko ya Sheria ni fursa ya kujenga taifa lenye haki na
usawa kwa wote
Kuhusu Tume ya Kurekebisha
Sheria Tanzania ni idara ya Serikali inayojitegemea chini ya Wizara ya Katiba
na Sheria ambayo imeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Tume ya Kurekebisha Sheria
Tanzania, Sura ya 171, na ilianza kazi rasmi tarehe 21 Oktoba, 1983. Kwa
mujibu wa sheria, Tume ina jukumu la kufanya mapitio ya sheria zote za Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania ili ziandane na mazingira ya wakati uliopo kwa
maendeleo endelevu.Mwanasheria Baraka Chipamba kutoka Tume hiyo, akitoa elimu kwa wanafunzi wa Chuo cha Walimu cha A3, Uuguzi na Uandishi wa Habari.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Nyumbu, Juma MMrope akizungumza wakati wa utoaji wa elimu hiyo.
Wanafunzi wa Chuo cha Walimu cha A3, Uuguzi na Uandishi wa Habari. wakipata elimu hiyo
Mwanasheria Vicky Mbunde, akisisitiza jambo wakati akitoa elimu kwa wanafunzi wa wa Chuo cha Walimu cha A3, Uuguzi na Uandishi wa Habari cha Kibaha mkoani Pwani.
Mwanasheria Baraka Chipamba kutoka Tume hiyo, akitoa elimu hiyo.
Wanafunzi wakiuliza maswali.
Picha ya pamoja
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Nyumbu wakipata elimu hiyo.