*Yamuomba Rais Kuongeza Utoaji wa Fedha Miradi ya Umwagiliaji
Dodoma. Kamati ya Kudumu ya Bunge, Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, imeridhishwa na maendeleo ya utekelezaji mradi wa Bwawa la Umwagiliaji Membe.
Bwawa hilo ambalo linajengwa na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), ujenzi wake umefikia asilimia 92 ya utekelezaji.
Wakizungumza leo Jumamosi Aprili 26, 2025 wajumbe wa kamati hiyo waliofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi huo, walisema NIRC inastahili pongezi kwa kutekeleza mradi huo kwa kiwango kikubwa na ubora.
“Tumeridhika na kitu kinachofanyika hapa, huu ni udhibitisho kwamba Tume ya Umwagiliaji inafanya kazi yake kwa ufasaha katika kuwahudumia wananchi,” alisisitiza Mwenyekiti wa kamati hiyo, Deodatus Mwanyika.
“Tunampongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kumshukuru kwa yale ambayo ameahidi katika ilani (Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025), ameyatekeleza kwa vitendo,” alisisitiza
Kwa mujibu wa Mwanyika, katika usimamizi wao kama wawakilishi wa wananchi wanatamani kuona matokeo na katika hilo wameyashuhudia maono ya Rais Samia.
Mwanyika alisema katika wizara ambazo Rais Samia ameziongezea fedha Kilimo ni moja wapo.
“Tunamshukuru ametusikia ndiye Rais pekee ambaye ameiinua wizara hii, awali bajeti yake ilikuwa Sh290 bilioni lakini sasa imefikia Sh1.2 trioni na katika hilo umwagiliaji imepata nyingi zaidi, karibu sh bilioni 400,” alieleza.
Alisisitiza Membe wanapendwa kwa kupel3kewa mradi huo na kusema kuna sababu za msingi kufqnya hivyo ikiwemo kulenga kuwanufaisha wananchi wengi zaidi kwa kutekeleza kilimo biashara.
“Waziri wa Kilimo, Hussen Bashe amefanya kazi nzuri, amepanga timu yake vizuri sana kuanzia Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na watendaji wake ndiyo maana leo tunaona utekelezaji wa miradi unaenda bila kusua sua. Hongera sana Mkurugenzi Raymond Mndolwa kwa kazi hii nzuri ya kutukuka, aliongeza.
Awali akitoa maelezo ya Mradi huo, Mkurugenzi Mkuu wa NIRC, Raymond Mndolwa alisema Bwawa hilo yenye uujazo wa bilioni 12 ambalo ligamwagilia hekta 2500 na likikamilika litanufaisha watu zaidi ya 1500.
Alisema mpaka sasa mradi huo umekamilika kwa zaidi ya asilimia 90 na unatarajia kukamilika mwishoni mwa Julai, 2025