Na.Alex Sonna _DODOMA
WAZIRI wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Adolf Mkenda amelitaka Shirika la Mtetezi wa Mama kuhakikisha Rais Samia Suluhu Hassan anashinda kwa kishindo katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Prof Mkenda ametoa kauli hiyo Leo Aprili 29,2025 Jijini Dodoma wakati akizungumza katika mkutano Mkuu wa Umoja wa Mtetezi wa Mama ambapo pia amezindua logo mbili zitakazotumiwa na Umoja huo katika shughuli zao.
Waziri Mkenda amesema mwaka huu ni wa chaguzi na Rais Samia anagombea kwa mara nyingine mara baada ya kupitishwa na CCM hivyo wana wajibu wa kuhakikisha anashinda kwa kishindo.
“Nawashukuru Mimi ni mwanachama mtiifu wa CCM nilikiwepo mkutano Mkuu wakati tukilipitisha jina la Mama Samia, tusipoteze muda tuna mgombea nae ni Samia Suluhu Hassan na mgombea mwenza na Zanzibar Dk Hussein Mwinyi hivyo tuwapigie kura,”amesema Waziri Mkenda.
Amesema anafurahi kwa kauli mbiu yao ya mitano tena baadae atakutana na Rais Samia atamweleza kuhusu Umoja huo..
Waziri Mkenda amesema uwekezaji mwanzo ulikuwa ni mdogo lakini kwa sasa uwekezaji ni mkubwa katika sekta ya Elimu kwani Rais Samia amehakikisha Kila kitu kwenye sekta hiyo kinakaa vizuri kwa kutoa fedha.
Amewataka kuendelea kuhimiza kuhusu umoja mshikamano kwani wao ni kioo Cha jamii.
“Tanzania imejengwa kwa misingi ya kushikamana nawapongeza sana na Mimi nitawaunga mkono.Kwa sababu kazi yetu ni kulea na sisi tutaangalia tunawashika mkono kwenye nini,”amesema Prof Mkenda.
Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja huo,Neema Karume amesema lengo la Umoja huo ni kumwinua mwanamke katika engo ya uchumi,pamoja na vijana kujadiliana mambo mbalimbali yanayohusu Nchi.
“Mheshimiwa Waziri hawa ni wapiga kura ambao wapo bega kwa bega na Mama lengo ni kuhakikisha anapata kura za kutosha katika uchaguzi Mkuu,”amesema Mwenyekiti huyo