.OR-TAMISEMI
Mkurugenzi wa Idara ya Afya Lishe na Ustawi wa Jamii, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Rashid Mfaume ameuelekeza uongozi wa kituo cha afya cha Buguruni *kudhibiti* mianya ya upotevu wa fedha katika kituo hicho ili kuendelea kuboresha miundombinu ya kituo na kufanikisha utoaji wa huduma kwa *wananchi* .
Dkt. Mfaume ametoa maelekezo hayo mara baada ya kutembelea na kukagua upatikanaji wa huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii katika kituo cha afya cha Mnazi Mmoja na kituo cha afya cha Buguruni.
“ *Tunapolenga* upatikanaji wa huduma za afya kwa ubora zaidi lazima *tudhibiti* mianya ya upotevu wa fedha na *kuongeza* mapato *kwa* kutoa huduma bora Kwa wateja wetu” amesisitiza
Aidha, Dkt. Mfaume ametaka timu ya *Usimamizi* wa *Huduma* za Afya (CHMT) katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam *kuongeza* usimamizi wa fedha katika kituo vituo mbalimbali katika Halmashauri hiyo.
Pia Dkt. Mfaume ameielekeza timu ya Usimamizi wa *Huduma* za Afya (CHMT) kushirikishana na Viongozi wa Serikali za Mitaa ili kufanikisha utoaji wa huduma chanjo Kwa Watoto katika Halmashauri hiyo.