Na Lucas Raphael,Tabora
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Deusdedith Katwale ameipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa shilingi billion 15 kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba .
Hali hiyo ilipelekea kuboresha na kuimarisha huduma za afya Mkoani humo na kupungua kwa malalamiko ya wateja na wananchi kwa ujumla.
Katwale alitoa kauli hiyo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha wadau wa bohari ya dawa kaada ya Tabora iliyofanyika katika ukumbi wa Jm Hotel manispaa ya Tabora mkoani hapa.
Alisema kwamba kutolewa kwa fedha hizo kumesabisha malalamiko ya ukosefu wa dawa kwenye mikutano ya hadhara kupungua kwa kiasi kikubwa, hiyo ni ishara kwamba huduma hivi sasa zimeimarishwa.
Mkuu huyo wa wilaya hiyo ya Tabora aliendelea kubainisha kwamba serikai baada ya kutoa fedha hizo hali ilipelekea huduma za afya kuboreshwa sana katika hospitali za Rufaa ya mkoa ,Hosptali za wilaya ,vituo vya afya na zahanati.
Alisema kwamba upatikanaji wa bidhaa za afya Mkoani humo umepanda hadi kufikia asilimia 89, hali inayotia matumaini, kwani huko nyuma hali haikuwa ya kuridhisha sana.
Aidha Katwale alipongeza utaratibu wa MSD kukutana na wateja na wadau wake, Ili kujadiliana namna bora ya kuboresha mnyororo wa bidhaa za afya nchini.
Hata hivyo alizitaka taasisi zingine kuinga kwa huandaa vikao kama hivyo kwa lengo la kupata mrejesho wa huduma wanazotoa kwa wadau wao.
Awali akieleza hali ya upatikanaji na usambazaji wa dawa kwa MSD katika kanda hiyo mkurugenzi wa huduma na uendeshaji Victor Sungusia alisema changamoto kubwa inayowakabili ni mazingira wezeshi ya kuhifadhia dawa pamoja na kuwafikia wateja wao hasa kipindi cha masika.
Kwa upande wake mganga mkuu wa mkoa wa Tabora Dkt Honoratha Rutatinisibwa aliwataka waganga wakuu wa wilaya na waganga wafawidhi kujadiliana na MSD ili vituo na hospitali zote zipatiwe dawa bila kujali kiwango cha madeni wanachodaiwa ili wananchi wasiumie kwa kukosa huduma za matibabu na dawa ..
Kaimu Meneja wa MSD Kanda ya Tabora Rashid Omary, alieleza majukumu ya Kanda hiyo, sambamba na eneo lake kiutendaji, wateja, sambamba na utekelezaji wa miradi mbalimbali wakati akitoa salamu za utangulizi kwenye kikao cha Wadau na Wateja wa MSD Kanda ya Tabora,
Kikao kazi cha siku moja wakiwa na kauli mbiu “ Tuzungumze Pamoja kutatua changamoto za upatinaji wa bidhaa za afya “