Waziri wa Madini,Anthony Mavunde bungeni wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara hiyo leo Mei 2,2025 bungeni jijini Dodoma kwa mwaka wa fedha 2025-2026.
Waziri wa Madini,Anthony Mavunde bungeni wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara hiyo leo Mei 2,2025 bungeni jijini Dodoma kwa mwaka wa fedha 2025-2026.
…….
WAZIRI ya Madini,imesema itaendelea na juhudi za kuwarasimisha na kuwaendeleza wachimbaji wadogo kwa kuweka mazingira wezeshi yatakayowahamasisha kufanya uwekezaji.
Hayo yameelezwa leo Mei 2,2025 bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Madini,Anthony Mavunde bungeni wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.
Mavunde Mavunde amesema Serikali itaendelea kuhamasisha taasisi za kifedha kutoa mikopo ya fedha na vifaa kwa wachimbaji wadogo.
Vilevile, kuboresha utendaji wa vituo vya mfano ili kuimarisha utoaji wa huduma na mafunzo kwa wachimbaji wadogo na kuimarisha huduma za uchorongaji kwa wachimbaji wadogo.
“Wizara pia itaimarisha utekelezaji wa mipango ya kuwawezesha wachimbaji wadogo ili waweze kufanya shughuli zao kwa tija kwa kuwatengea maeneo na kuwapatia leseni kwenye maeneo ambayo yana taarifa za jiolojia.
“Kuhamasisha wachimbaji wadogo kushiriki mikutano, maonesho na makongamano mbalimbali ndani na nje ya nchi kwa lengo la kujifunza na kutangaza shughuli zao,”amesema Mavunde
Mavunde amesema pia Wizara inaendelea uhamasisha wachimbaji wadogo kushiriki kwenye minada na maonesho ya madini.