MKUU wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo ,amesema mradi wa kuboresha miundombinu ya jiji( DMDP) awamu ya pili unatarajia kujenga Barabara za urefu km 67 Wilayani Ilala ,barabara hizo za kisasa zitawekwa lami na kufungwa taa.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam mkuu wa wilaya Edward Mpogolo, alisema mradi huo wa DMDP ukikamilika utatatua sehemu ya changamoto katika baarabara ambazo zimekuwa kero maeneo tofauti .
“Mradi wa awamu ya pili wa DMDP barabara za urefu wa KM 67utakomboa wilaya ya Ilala itakuwa ya kisasa kama ulaya ndogo jiji letu litapendeza, tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi ambapo ndani ya wilaya yetu hizi barabara zitakuwa mkombozi kwa wananchi mradi ukikamilika.
Alitaja moja ya barabara zinazojengwa kwa lami katika mradi wa DMDP Kitunda_ Kivule njia nne kwa sasa Mkandarasi wa Mradi wa DMDP yupo kazini na maeneo yenye changamoto ya mashimo atayaboresha .
Aidha alisema barabara Kimanga Mazda ina urefu wa km 3 itajengwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 na Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam na TARURA inajengwa kwa kiwango cha lami mita 500 na zege katika daraja la Kimanga.
Alisema barabara korofi za TABATA Kimanga mpango wa kuzifanyia matengezo katika mashimo umekamilika ,na baada mvua Mkandarasi atamalizia .
Alitaja barabara zingine zitakazojengwa kwa kiwango cha lami Pugu Majohe mbondole njia nne ina urefu wa Kilometa 12 .6 inafanyiwa usanifu itajengwa kwa kiwango cha lami katika bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 na eneo la Halisi kata ya Majohe itajengwa kwa kiwango cha ZEGE mita 400 na eneo litakalobaki litakarabatiwa kwa kiwango cha changarawe