Happy Lazaro, Arusha .
Benki ya CRDB imetoa kiasi Cha shilingi milioni (385,000,000),kwa vikundi vitano vya wanawake na vijana mkoani Arusha.
Akizungumza katika semina ya vikundi vya wajasiriamali zaidi ya 130 vilivyohudhuriwa na watu takribani 1,000 ,Mkuu wa kitengo cha biashara kutoka benki ya CRDB ,.Boma Raballa amesema kuwa benki hiyo imeshatoa mikopo yenye jumla ya shilingi trilioni 10.946 kwa sekta zote hapa nchini kwa wajasiriamali wa Awali na Kati.
Amesema kuwa ,mikopo hiyo ambayo ipo chini ya Taasisi Tanzu ya CRDB Foundation kupitia programu ya Imbeju imelenga kuwanufaisha wanawake na Vijana ili kuboresha maisha yao.
Raballa amesema kuwa kupitia Taasisi Tanzu ya CRDB Foundation jumla ya mitaji wezeshi yenye thamani ya shilingi bilioni 20 imeshatolewa na wanufaika wakubwa ni Wanawake na Vijana.
“Hii mikopo ni utekelezaji wa ilani ya chama Cha mapinduzi na mtazamo sahihi wa serikali wa kuhakikisha kuwa inatafuta namna Bora ya kuisaidia jamii kukuza kipato cha mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla kupitia mikopo hii”amesema .Raballa
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Joseph Modest Mkude ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema kuwa semina hiyo ni muhimu na ni Juhudi za serikali ya Awamu ya Sita chini ya Raisi Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuboresha maisha ya wananchi kwa kutoa kipaumbele kwa Wanawake na Vijana.
Amesema kuwa Ushauri na Mafunzo ya namna ya kukuza biashara kutoka kwa wataalamu hao ni miongoni mwa sehemu ya uhakika za kupata elimu ya fedha na kufanikisha mipango Yao.
“Uwepo wa Taasisi ya CRDB Foundation hapa Arusha Leo ni fursa kwa Wanawake na Vijana Wetu kuelimika na kufanya biashara kwa malengo makubwa, ambayo yatafanikiwa kukuza kipato binafsi,kaya na taifa kwa ujumla naomba muendelee kushirikiana na benki hii”amesema Mkude .
Mkude amewataka kutumia fursa hiyo kwa kuwa ni adimu na kuitumia vyema katika kuwa mahiri katika biashara na maisha kwa Ujumla,kwa kuwa elimu ya fedha ni ngao ya kukabiliana na umaskini ambao kila mmoja anauchukia.
“Programu hii ya Imbeju ambayo ipo chini ya Taasisi Tanzu ya CRDB Foundation Ina lengo la kusaidia Wanawake,Vijana na Makundi Maalumu ili kuboresha maisha Yao na uchumi kwa ujumla.”amesema Mkude.