Picha ya pamoja kati ya Chuo cha Furahika na Chuo cha afya cha Mchukwi mara kusaini makubaliano.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mchukwi, Dkt Japhet Guzuye akizungumza kuhusiana na umuhimu wa kuanzishwa kampansi kutokana na uhitaji wa rasilimali watu katika sekta ya afya.
Mkuu wa Chuo cha Furahika Dkt.David Msuya wakibadilishana hati za Makubaliano na Mkuu wa Chuo Uuguzi na Ukunga cha Mchukwi Kibiti Malsel Daniel.
Mkuu wa Chuo cha Uuguzi Mchukwi, Malsel Daniel akizungumza kuhusiana na kusogeza huduma kwa wananchi kusoma kozi ya Uuguzi na Ukunga katika Kampensi mpya ndani ya Chuo cha Furahika.
Mkuu wa Chuo Cha Ufundi Furahika Dkt. David Msuya akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na makubaliano katika Chuo cha Furahika kuanzishwa Kampasi ya Chuo cha Uuguzi na Ukunga Mchukwi wilayani Kibiti katika Chuo cha Furahika jijini Dar es Salaam.