Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Mei 20, 2025 ameshiriki kwenye zoezi la kuboresha taarifa zake kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura Ikwiriri – Rufiji.
Mara baada ya kuboresha taarifa zake, Mhe. Mchengerwa amewataka wananchi kote nchini kutumia muda wa siku mbili zilizobaki kuboresha taarifa zao.
” Naomba kutoa wito kwa wananchi kwenda kuboresha taarifa zao katika kipindi hiki kifupi cha siku mbili ili waweze kupata haki yao ya msingi ya kupiga kura kwa maendeleo ya taifa letu” amesisitiza Mhe waziri
Aidha, amefafanua kuwa zoezi la kuboresha taarifa ni la muhimu kwa kuwa taarifa hizo zinaweza pia kutumika na Serikali ili kuleta maendeleo.
Pia Waziri Mchengerwa ametoa wito kwa watanzania kutumia vizuri hali yao ya kupiga kura wakati utakapofika.