ππ. ππππ‘ππ₯π€ πππ¨π¨ππ£
Hifadhi ya Taifa Ruaha inazidi kuitangaza Tanzania kimataifa baada ya kutajwa na Newsbytes Jukwaa la Kimataifa linalojihusisha na utoaji wa taarifa za utalii, mazingira na maendeleo kuwa miongoni mwa maeneo matano ya safari yasiyojulikana sana barani Afrika lakini yenye vivutio vya kipekee kupitia makala ya βHidden Gems: 5 Lesser-Known Safari Destinations.β
Ruaha, ambayo ni miongoni mwa hifadhi kubwa zaidi barani Afrika imekuwa chaguo bora kwa watalii wanaotaka kutalii maeneo yasiyo na msongamano wa watalii. Hifadhi hii inajivunia kwa kuwa na makundi makubwa ya Tembo, Simba, Nyati, Swala pamoja na mandhari ya kuvutia yenye mchanganyiko wa uoto wa asili Miombo na Savana, milima, bonde la Usangu lenye bioanuwai adimu pamoja na chanzo cha mto βThe Great Ruahaβ, hifadhi isiyo na msongamano mkubwa wa watalii vilevile na shughuli za kibinadamu.
Maeneo mengine yaliyoorodheshwa katika makala hiyo kuwa ni βhazina zilizojifichaβ ni pamoja na Luangwa Valley (Zambia), Skeleton Coast (Namibia), Tuli Block (Botswana), na Andasibe-Mantadia (Madagascar).
Maeneo yaliyohifadhiwa ikiwemo Hifadhi ya Taifa Ruaha yana umuhimu mkubwa katika kulinda bioanuwai, vyanzo vya maji yanayotiririka kuelekea mabwawa mbalimbali ya kuzalisha umeme na kutoa nafasi kwa jamii zilizopo jirani na hifadhi kunufaika kupitia shughuli za utalii.Β
Serikali ya Tanzania, chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ameendelea kuhamasisha utalii kupitia filamu ya Tanzania βThe Royal Tour na Amazing Tanzaniaβ zinaendelea kuvutia watalii wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani na kuendelea kuitambulisha Tanzania kimataifa.
Juhudi za Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) zimeleta matokeo chanya katika sekta ya utalii nchini Tanzania ambapo kwa sasa sekta ya utalii inachangia zaidi ya asilimia 17 katika Pato la Taifa. Hii ni ishara ya mafanikio ya sera na mikakati ya kuendeleza utalii endelevu unaolinda mazingira na kuongeza ajira kwa Watanzania.
Kutajwa kwa Hifadhi ya Taifa Ruaha ni ushahidi wa mchango mkubwa katika maendeleo ya sekta ya uhifadhi na utalii na pia ni wito kwa watalii wa ndani na nje kuendelea kuichagua Ruaha kama eneo bora la kutembelea na kujionea vivutio vya utalii katika mazingira yake asilia (Pristine nature).
βΒ