Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) ameshiriki na kuhutubia Kongamano lililoandaliwa na Taasisi ya PPRA lililolenga kujadili Ununuzi wa umma na Ukuzaji wa kampuni za wazawa na makundi maalum kwa ukuaji wa Uchumi Jumuishi katika zama hizi za mabadiliko ya teknolojia/ Kidigitali lililofanyika Jijini Arusha Juni 16, 2025.
Katika hotuba yake, amekumbushia umuhimu wa kuendelea kutambua kuwa mabadiliko mbalimbali yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dr. Samia Suluhu Hassan , Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yanalengwa pamoja na mengineyo kuwasaidia na kukuza ustawi wa Watu wenye mahitaji maalum.
Pia alikumbusha mambo 6 yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita katika kuwawezesha vijana na watu wenye ulemavu ili waweze kujiinua kiuchumi ikiwemo maelekezo ya kisheria ya kuendelea kutenga Asilimia 30 ya zabuni za ununuzi wa umma.
Pia umuhimu wa kutoa elimu na kuwashirikisha wadau muhimu katika jamii wakiwemo Madiwani na Wakurugenzi wa Halmashauri, Manispaa na Majiji ili elimu ya kuwepo kwa fedha maalum zinazotengwa toka kwenye manunuzi ya Umma ijulikane kwani moja ya changamoto kubwa kwa sasa ni ufahamu hafifu wa kuwepo kwa fedha hizi. Umuhimu na msisitizo kama huu umesaidia sana vijana, wanawake na wenye ulemavu kukimbilia zile asilimia 10 zinazotengwa na Halmashauri kutoka kwenye mapato ya ndani.
Alimaliza kwa kuwashukuru sana PPRA kwa kazi nzuri na kutambua umuhimu wa kuandaa kongamano hili ambalo kwa hakika linalenga kuwawezesha wananchi. Kwani kufikia kwa malengo haya ni kuwawezesha Watanzania.