Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene akitazama betri la moyo “Pacemaker” wanalowekewa wagonjwa ambao mapigo yao ya moyo yako chini ya asilimia 50 alipotembela banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.
Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene akitazama valvu ya moyo wanayowekewa wagonjwa ambao valvu zao hazifanyi kazi vizuri alipotembela banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Ghati Chacha akimkabidhi Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene folder lenye taarifa za taasisi hiyo wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Juma Mkomi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) alipotembelea banda la taasisi hiyo leo wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Juma Mkomi akizungumza na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Ghati Chacha alipotembelea banda la taasisi hiyo leo wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.Picha na JKCI