Kamishna Msaidizi wa kitengo cha maendeleo ya biashara TANAPA ,Jully Lyimo akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha


…………
Happy Lazaro, Arusha .
Mamlaka ya hifadhi ya Taifa TANAPA imeeleza kunufaika na maonesho ya kitalii.ya KARIBU-KILIFAIR yanayofanyika jijini Arusha kwa kutangaza vivutio vya utalii na kupata fursa ya kutangaza hifadhi zao mbalimbali kwa wageni wengi ambao wanatamani kutembelea hifadhi hizo .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha kwenye maonesho hayo ,Kamishna Msaidizi wa kitengo cha maendeleo ya biashara TANAPA ,Jully Lyimo amesema kuwa maonesho hayo yameiuwa na tija kubwa sana kwao kwa kuweza kutangaza vivutio vyao mbalimbali.
:Tumekuwa na siku tatu kubwa za mafanikio katika sekta ya utalii ambapo wizara ya maliasili na utalii imeshiriki.maonesho kikamilifu pamoja na shirika la hifadhi Tanapa ,tumeona kuna uwakilishaji mkubwa wa kuweza kuonyesha vivutio mbalimbali vinavyopatikana katika hifadhi zetu za Taifa Tanzania na pia tumekutana na mawakala mbalimbali wa kutoka ndani na nje ya nchi ambao wamekuja kupata taarifa mbalimbali kuhusiana na vivutio vinavyopatikana katika hifadhi za Taifa na fursa kiuwekezaji.”amesema Jully .
Amesema kuwa baada ya maonesho haya kwa mwaka unaofuata wataongezeka idadi ya watalii wa kutoka ndani ya nchi kanda ya Afrika Mashariki na kutoka pia Afrika na dunia nzima kwa kuwa wameweza kutoa taarifa ambazo zingine labda mawakala wao walikuwa hawazifahamu vizuri.
“Tumeuza na tumejikita sana kuuza hifadhi za kusini na Magharibi ambazo kwa nafasi kubwa hazina watalii wengi wanaotembelea ingawa ina vivutio vingi lakini watalii wake bado wanaendelea kukua na bado ni wachache ikilinganishwa na hizi hifadhi za kaskazini.”amesema Jully .
“Kwa ujumla tumepata kuuza hifadhi zetu wageni wengi walikuwa wanaulizia na kushangaa hifadhi ya Taifa ya kitulo watu wanapenda kutembelea utalii wa wanyama na wangependa kujua hivyo kupitia maonesho hayo wamepata elimu nzuri.”amesema .
Akizungumzia hifadhi ya Taifa ya Katavi ambayo ipo upande wa Magharibi ya nchi na ina vivutio vingi sana ambavyo ni vya kujivunia na ina fursa nyingi sana za kiuchumi na uwekezaji mbazo mawakala wameweza kuzijua na kuzitambua na kuweza kuhasika kwenda kupeleka watalii upande huo wa hifadhi hizo .
“Kupitia kujitangaza huko tunaamini watalii watakuja na kuongeza idadi kubwa ya wageni kutoka ndani na nje ya nchi na wageni wa nje ya watanzania kupitia maonesho haya.”amesema .
“Tunaamini kuwa tutakuwa na wawekezaji wataongezeka kwa hii miaka inayoenda usoni kwani wengi wametamani kwenda kutembelea maeneo.”ameongeza .
Kwa upande wake Askari wa uhifadhi idara ya utalii kutoka hifadhi ya Taifa Burungi Chato Emmanuel Nyundo amesema kuwa, wamefika.kwenye maonesho hayo kwa lengo la kuelemisha wadau wa utalii pamoja na wananchi wenye nia ya kutaka kutembelea na kuwekeza katika hifadhi hiyo .
“Tunawakaribisha kwani fursa za uwekezaji zipo nyingi sana kwani hifadhi ni kubwa na ina vivutio vingi sana na ina maziwa ya kutosha pamoja na ziwa kubwa la Victoria ambapo sehemu.sehemu yake ipo ndani ya hifadhi hiyo hivyo ni vizuri wageni wakatembelea kwani wana vivutio vya kutosha na fursa za uwekezaji kwani maeneo ya uwekezaji bado yapo .”amesema .
Naye Askari wa jeshi la uhifadhi daraja la pili hifadhi ya Raifa Katavi Sabo Lucas
amesema kuwa, hifadhi hiyo inasifika.kwa makundi makubwa sana na viboko kwani ni hifadhi ambayo utaweza kumwona kiboko kirahisi kuliko hifadhi zingine zote kwa hapa Tanzania na wanasifika pia kwa makundi makubwa ya nyati ,Tembo , Simba wengi na wanyama jamii ya swala pamoja ndege wanaopatikana maeneo ya kwenye maji hivyo, amewataka wananchi kufika kwa wingi kujionea vivutio vinavyopatikana katika hifadhi hiyo.