Afisa mauzo wa Shirika la Nyumba NHC Mariam Chisumo akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea katika banda la NHC katika maomesho ya wiki ya Utumishi wa Umma yanayoemdelea Kwenye viwanja via Chinangali Parks jijimi Dodoma.
Abbu Ahmed Mwangu wa Shirika LA Nyumba NHC akitoa. maelezo kwa wananchi waliotembelea katika banda la NHC katika maomesho ya wiki ya Utumishi wa Umma yanayoemdelea Kwenye viwanja via Chinangali Parks jijimi Dodoma.
………………
Dodoma, Juni 17, 2025
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Boniface Simbachawene, amesema kuwa watumishi wa umma ndio uti wa mgongo wa utekelezaji wa sera na mipango ya maendeleo ya taifa, hivyo wanapaswa kuwajibika kwa weledi, uadilifu na uzalendo mkubwa.
Akizungumza wakati akifungua Wiki ya Utumishi wa Umma inayofanyika jijini Dodoma Shirika la Nyunba NHC likiwa miongoni mwa mashirika ya serikali yanayoshiriki kikamilifu katika maadhimisho hayo kuitangaza miradi yake, Waziri Simbachawene alisisitiza kuwa Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya kazi na maslahi ya watumishi wa umma ili kuongeza tija na ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
“Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imeweka mkazo mkubwa katika kuboresha utumishi wa umma. Hii ni pamoja na kuongeza ajira, kupandisha vyeo, pamoja na kulipa stahiki mbalimbali kwa wakati,” alisema Simbachawene.
Ameeleza kuwa kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu – “Ubunifu na Matumizi ya TEHAMA katika Kuboresha Huduma kwa Umma” – inalenga kuhimiza taasisi za umma kutumia teknolojia ili kufanikisha utoaji wa huduma kwa haraka, kwa gharama nafuu na kwa viwango vinavyokubalika.
Waziri pia aliwataka watumishi wa umma kujitathmini na kujirekebisha pale panapobainika changamoto, huku akisisitiza kwamba Serikali haitasita kuchukua hatua kwa yeyote atakayekiuka maadili ya utumishi wa umma.
“Tunataka kuona watumishi wa umma wanakuwa sehemu ya suluhisho, si chanzo cha kero kwa wananchi,” aliongeza.
Waziri Simbachawene Amewasihi wakazi wa Dodoma na mikoa ya jirani kukaribia katika maonesho ya wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea kwenye viwanja vya Chinangali Parks ili kupata elimu na huduma zinazotolewa na wizara na taasisi mbalimbali za Umma ambazo, zitatolewa katika maonesho yanayoendelea kwenye viwanja vya Chinangali parks
Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na viongozi waandamizi wa serikali, wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, na baadhi ya wananchi waliopata fursa ya kufahamu huduma mbalimbali zinazotolewa na taasisi za umma kupitia maonesho maalum.
Wiki ya Utumishi wa Umma huadhimishwa kila mwaka kuanzia Juni 16 hadi 23, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa watumishi wa umma barani Afrika na kuhamasisha uwajibikaji katika kutoa huduma kwa umma.