NA DENIS MLOWE IRINGA
MKURUGENZI wa Masoko wa Kampuni ya VunjaBei Fadhili Fabian Ngajilo leo rasmi amechukua fomu ya kugombea ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini kwa mara ya tatu kupitia chama hicho na kunena nia ya kugombea.
Akizungumza na waandishi wa habari Ngajilo baada ya kuchukua fomu hiyo kwenye ofisi kuu ya Ccm wilaya ya iringa mjini na kukabidhiwa na Katibu wa Ccm wilaya ya Iringa mjini Hassan Makoba amekishukuru chama cha mapinduzi CCM kwa kupata fursa kwa kumpatia fomu huku akiweka wazi kuwa hakuna chama chenye kuleta maendeleo kama chama cha Mapinduzi CCM.
Ngajiro alisema kuwa ana dhamira ya dhati ya kuwatumikia wana Iringa akiomba wana CCM kumuamini huku akiweka wazi kuwa ni mara yake ya tatu kufukuzia mbio hizo na huu ni wakati sahihi wa kuwatukia wanaIringa kwa kuwa uzoefu anao.
Aidha amesema anao Uzoefu wa kutosha ndani ya chama na serikali na amejipima na kuona ana sifa zote za kugombea jimbo la Iringa mjini kwa kuwa anajua changamoto za jimbo la Iringa mjini hivyo yuko tayari kushirikiana na wananchi kuleta maendeleo.
Katibu wa CCM wilaya ya Iringa Mjini Hassan makoba amesema kwa watia nia wote waliochukua fomu ni lazima wafuate misingi na kanuni ya chama kuepuka kuanza kampeni kabla ya muda huku akisisitiza kuwa uchuaji wa fomu umeanza rasmi leo juni 28 na kurejesha mwisho july 2 saa kumi jioni.
Ngajilo ni mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi mkoa wa Iringa ambapo tayari ameandika barua kwa chama chake cha mapinduzi kuachia nafasi hiyo kwa muda ili kuingia kwenye mchakato huo wa kutia nia jimbo la Iringa Mjini