Umoja wa Wadau wa maendeleo wenye asili ya Makete waishio nje ya wilaya Hiyo mkoani Njombe wamelazimika kuchangishana fedha na kisha kununua mashine za kuhifadhi watoto wanaozaliwa kabla ya wakati(njiti)pamoja na kemikali kwa ajili ya matumizi ya maabara ambazo zilizogharimu kiasi cha mil 70 huku lengo likiwa ni kumaliza tatizo vifo vya watoto njiti ambavyo hutokea mara kadhaa kwasababu ya na uhaba wa mashine za kuhifadhia watoto hao pindi tu wanapozaliwa.
Awali akieleza hali ilivyo wakati wa makabidhiano ya msaada huo, Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Makete Dr Ligobert Kalisa ambae pia ni kaimu mkurugenzi halmashauri hiyo na Elizabeth Lulandala afisa muuguzi msaidizi hospitali ya wilaya Makete wamesema kwamba Hospitali nyingi za wilaya hiyo ikiwemo hospitali ya wilaya zinachangamoto ya mashine za kuhifadhi watoto njiti hivyo kuanzia sasa tatizo limepatiwa muarobaini na wadau hao na kisha kuomba watu wengine kuguswa kufanya hivyo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa umoja wa watu wenye asili ya Makete waishio nje Dr Toba Nguvila na amesema waliguswa kusaidia vifaa hivyo baada ya kuelezwa ukubwa wa tatizo na kwamba kinachotakiwa ni kuvitunza na kutumia ipasavyo ili vinufaishe wahusika.
Nae Monny Luvanda ambae ni Katibu wa Umoja wa Wadau wa Maendeleo Makete amesema umoja huo ulilazimika kutafuta fedha baada ya kuambiwa watoto wengi wanaozaliwa kabla ya wakati wanapoteza maisha kwasababu ya kutokuwa na mashine maalumu za kuwahifadhi jambo ambalo limekuwa chanzo cha wilaya hiyo kuwa na idadi ndogo ya watu.
wamesema ,wamelazimika kufanya hivyo ili kurejesha furaha nyumbani ili kuokoa maisha ya vizazi vijavyo.
Aidha wadau hao akiwemo Sessilia Msafiri na Suzan Mbilinyi wamesema wataendelea kutafuta muarobaini wa changamoto ya huduma za jamii Makete hadi pale zitakapo kwisha huku changamoto ya matumizi ya tehama mashuleni na uhaba wa mashine za kuhifadhi watoto njiti zikipewa kipaumbele zaidi.
Umoja wa wana Makete waishio nje pia umepokea ombi la Compyuter kwa ajili ya maabara ya tehama na kisha kuahidi ifikapo Desemba zitaletwa.



