Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Bw. Lazaro Twange amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa kituo cha kupoza umeme cha Kiloleni kilichopo Mkoani Tabora ambapo amesema Mradi huo umefikia asilimia 80.
Bw. Lazaro Twange amefanya ziara hiyo Julai 4 2025 akiwa ameongozana na Meneja wa Kanda ya Magharibi Mhandisi. Richard Swai pamoja na Meneja wa Mkoa wa Tabora Mhandisi Amina Ng’imba ambapo amesema amerishishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huo ambao hadi kukamilika kwake unatarajia kutumia kiasi cha shilingi bilioni 14.6.
Amesema Kituo cha kupoza umeme cha Tabora mjini kilichopo eneo la kiloleni Manispaa ya Tabora ni miongoni mwa vituo tisa vya kupoza umeme hapa nchini vinavyofanyiwa marekebisho ikiwemo uboreshaji wa miundombinu kupitia mradi wa TT group ili kuzalisha umeme wa uhakika na kuwaondolea adha wananchi.
Katika ziara hiyo Bw. Twange pia alipata nafasi ya kuzungumza na wafanyakazi wa TANESCO Mkoani Tabora ambapo amewapongeza Kwa utendaji wa kazi mzuri huku akiwasisitiza kuendelea kufanya kazi Kwa weledi, upendo na mshikamano.