…………………
Na Neema Mtuka Sumbawanga
Rukwa :Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Rukwa limewataka wateja wanaodaiwa kulipa madeni yao ili kuwezesha huduma kwa wananchi.
Akizungumza katika kikao kazi cha TANESCO Mkoa wa Rukwa na Waandishi wa Habari Julai 6 2025, Meneja TANESCO Mkoa wa Rukwa Mhandisi Johnson Mwigune amesema kuwa mpango wa shirika hilo ni kuhakikisha kila Mwananchi anapata umeme popote alipo na hivyo Wateja wanaodaiwa wanapaswa kulipa madeni yao ili kuwezesha upatikanaji wa huduma bora kwa wateja .
Mwigune amesisitiza kuwa Wananchi wanapaswa kulinda miundombinu ya umeme kwa maendeleo ya sasa na kizazi cha baadae.
Kwa upande wake afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja TANESCO Mkoa wa Rukwa Angeline Bidya amesema kuwa Jamii inapaswa kuacha tabia ya kuchoma moto wakati wa kusafisha mashamba ili kuepuka uharibifu wa miundombinu ya umeme.
“Ni muhimu wananchi wailinde miundombinu ya umeme na waache tabia ya kujiunganishia umeme bila kufuata utaratibu wa Shirika” amesema.
Aidha Mhandisi Mwigune ametoa onyo kali kwa baadhi ya wananchi wanaojiita vishoka kuacha tabia ya kufanya kazi za Shirika hilo na kuwa ni kinyume na sheria za nchi.
Amewasisitiza wananchi kutoa taarifa pindi wanapowaona vishoka ambao wanafanya kazi za tanesco kinyume na taratibu waweze kutoa taarifa ili wachukuliwe hatua stahiki.
Afisa uhusiano huduma Kwa wateja Tanesco Mkoa wa Rukwa akizungumzia namna wanavyo hudumia wateja