Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi – Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), Bernadetta Ndunguru akiwahudumia wateja waliotembelea Banda la NACTVET katika maonesho ya 49 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Sabasaba)Jijini Dar es Salaam.
Afisa Uhusiano wa NACTVET Dora Tesha akiwahudumia wateja waliotembelea Banda la NACTVET katika maonesho ya 49 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Sabasaba)Jijini Dar es Salaam.
Wateja wakipata maelezo katika Banda la NACTVET katika Maonesho ya 49 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Sabasaba)Jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
MWENYEKITI wa Baraza la Uongozi – Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), Bernadetta Ndunguru amesema kuwa Baraza hilo linaratibu Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi katika kuwaandaa vijana kuwa na ujuzi wa kuweza kujiajiri na kuajiriwa.
Akizungumza katika kwenye banda la NACTVET kwenye maonesho ya Sabasaba, Bi. Ndunguru amesema nchi inaingia katika uchumi wa kati ambao unatokana na kuwepo viwanda vingi ambavyo vinahitaji mafundi mahiri, hivyo Baraza limejidhaititi katika kuhakikisha vyuo vinazalisha nguvukazi yenye ujuzi itakayoweza kuhudumia viwanda hivyo.
Amesema NACTVET imeshiriki maonesho hayo ili kutoa elimu kuhusu shughuli zinazofanywa na Baraza na kupokea mrejesho kutoka kwa wadau wake.
Bi. Ndunguru amesisitiza kuwa NACTVET inaendeleza mikakati ya kuhakikisha wahitimu wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi wanakidhi viwango vya ndani pamoja na nje ya nchi.
Benadetta amesema kuwa Serikali ya Awamu ya sita imeweka msukumo katika viwanda hivyo vinahitaji nguvu kazi ya vijana wa kitanzania