Na Sophia Kingimali.
Mkurugenzi mkaazi wa taasisi ya CNV TANZANIA Jeen Kootsra amesema wakulima nchini wanapaswa kujengewa uwezo ili kuweza kutambua namna bora ya kufanya kilimo himilivu kwa kuzingatia mabadiliko ya Tabia nchi ili kuweza kuongeza uzalishaji lakini kujiongezea kipato.
Hayo ameyasema leo Julai 17,2025 wakati wa uzinduzi wa Muongozo wa mafunzo ya hali ya hewa ambapo muongozo huo uliandaliwa tangu 2017 wakati SNV iliposhirikiana na wizara ya maendeleo ya Uholanzi pamoja na ubarozi wa Tanzania,kenya na Uganda.
“Wazo la mradi wa Craft ni kujenga uvumilivu wa hali ya hewa katika mifumo ya kilimo cha chakula kwa nchi hizi tatu kwa kushirikiana na sekta binafsi’,Amesema.
Akizungumzia mradi huo wa craft Afisa tathimini nq ufuatiliaji mradi wa SNV TANZANIA Sophia Kessy amesema wamekuwa wakitekeleza kwa kushirikiana na makampuni ya wajasiliamali wa kati na wadogo pamoja na vyama vya wakulima wadogo ili kuweza kuwafikia wakulima hao.
Aidha amesema muongozo huo uliozinduliwa utatumika kutoa mafunzo na kutumika na wadau ambao wapo katika sekta ya kilimo ambao wanawafikia wakulima popote walipo katika mikoa yao.
“Muongozo huu unambinu zote za kuweza kufanya kilimo himilivu na teknolojia ili kuweza kumfanya mkulima mdogo kuongeza uzalishaji lakini pia kuongeza kipato tumekuwa tukiwafikia wakulima wadogo kwa kuwapa mafunzo na mbinu za kuweza kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi”,Amesema.
Kwa upande wake mtafiti kiongozi zao la viazi Mvuringo kutoka Taasisi ya utafiti wa kilimo TARI kituo cha Uyole Owekisha Kwigizile amesema kwa kutumia kilimo bora kinachotumia teknolojia na kuzingatia mabadiliko ya tabia ni kichocheo cha ungezeko la chakula nchini.
“Sisi kama TARI tawi la Uyole tumetekeleza miongozo inyotutaka kusaidia wakulima kijifunza namna ya bora ya kulima na kuwa na kilimo chenye tija kwa maslahi yao binafsi lakini kwa maslahi ya Taifa kwa ujumla”Ameaema.
Kwa upande wake Hance Melcheor Mratibu wa miradi kutaka EA FOODS LIMITED ambae ni mnufaika wa mafunzo yanayotolea na SNV amelipongeza shirika hilo huku akiwataka kuendelea kuwasaidia na wakulima wengine kupata mafunzo hayo ili waweze kulima kwa tija.
“Kiukweli kupitia mafunzo haya tunayopewa na SNV kuliyiabpamoja na kutufadhili pembembejeo imetusaidia sana kwani kilimo chetu kimeimarika tulikuwa tunapata Tani 4 kwa ekari lakini sasa tunapata mpaka tani 8 kwa ekari mimi niwaombe mafunzo haya yawe endelevu lakini pia muwafikie na wakulima wengine ili nao waweze kufaidika”,Amesema.