Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akieleza kuhusu Serikali kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Ubeligiji, alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ubeligiji nchini Tanzania, Mhe. Peter Huyghebaert, Ofisi ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
Na. Peter Haule, WF, Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ubeligiji nchini Tanzania, Mhe. Peter Huyghebaert, ambapo wamezungumza kuhusu kuendeleza ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na nchi hiyo.
Mkutano huo uliofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam, ulihudhuriwa pia na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Melckzedeck Mbise, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ubeligiji, Bw. Koenraad Goekint na Mkuu wa Masuala ya Ushirikiano wa Ubeligiji, Bi. Fanny Heylen pamoja na wajumbe wengine kutoka Wizara ya Fedha na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akiagana na Balozi wa Ubeligiji nchini Tanzania, Mhe. Peter Huyghebaert, baada ya mkutano kati yao kuhusu ushirikiano katika sekta mbalimbali za maendeleo kati ya Tanzania na nchi hiyo, uliofanyika, Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akieleza kuhusu Serikali kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Ubeligiji, alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ubeligiji nchini Tanzania, Mhe. Peter Huyghebaert, Ofisi ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ubeligiji, Bw. Koenraad Goekint, akieleza kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo, wakati wa Mkutano kati ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Balozi wa Ubeligiji nchini Tanzania, Mhe. Peter Huyghebaert (kulia), Ofisi ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Ubeligiji nchini Tanzania, Mhe. Peter Huyghebaert, akieleza jitihada za nchi yake katika kuharakisha maendeleo, wakati wa mkutano na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (wa pili kulia), ukiwa katika Mkutano na Ujumbe wa Serikali ya Ubeligiji, ukiongozwa na Balozi wa Ubeligiji nchini Tanzania, Mhe. Peter Huyghebaert (haupo pichani), Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Melckzedeck Mbise (kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano kati ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (wa pili kulia), na Balozi wa Ubeligiji nchini Tanzania, Mhe. Peter Huyghebaert (wa pili kushoto), Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
Ujumbe wa Serikali ya Ubeligiji, ukiongozwa na Balozi wa Ubeligiji nchini Tanzania, Mhe. Peter Huyghebaert (katikati), ukiwa katika Mkutano na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (hayupo pichani), Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akiongoza Mkutano kati yake na Balozi wa Ubeligiji nchini Tanzania, Mhe. Peter Huyghebaert, Ofisi ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (wa tano kulia) na Balozi wa Ubeligiji nchini Tanzania, Mhe. Peter Huyghebaert (wa nne kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Tanzania na Ubeligiji, baada ya mkutano kati yao kuhusu ushirikiano wa Maendeleo, Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha)