MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Kenani Kihongosi, akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 20,2025 jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo mkoani humo kwa kipindi cha miaka minne chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa Idara ya Habari (MAELEZO) kutoa fursa kwa Wakuu wa Mikoa kueleza mafanikio yaliyopatikana kwenye maeneo yao.
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Kenani Kihongosi, akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 20,2025 jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo mkoani humo kwa kipindi cha miaka minne chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa Idara ya Habari (MAELEZO) kutoa fursa kwa Wakuu wa Mikoa kueleza mafanikio yaliyopatikana kwenye maeneo yao.
SEHEMU ya Waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Kenani Kihongosi, (hayupo pichani) wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo mkoani humo kwa kipindi cha miaka minne chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa Idara ya Habari (MAELEZO) kutoa fursa kwa Wakuu wa Mikoa kueleza mafanikio yaliyopatikana kwenye maeneo yao.
Na.Alex Sonna-DODOMA
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kenani Kihongosi amesema katika Kipindi cha miaka Minne cha Serikali ya awamu ya Sita,Mkoa wa huo umepiga hatua kubwa katika sekta ya Afya ambapo Serikali imetoa jumla ya shilingi Bilioni 94.2 kwa ajili ya kuboresha huduma za afya kwa kujenga na kuboresha miundombinu ya afya, ununuzi wa dawa na vifaa tiba.
Mhe.Kihongosi,ameyasema hayo leo, Julai 20, 2025, jijini Dodoma, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo mkoani humo kwa kipindi cha miaka minne chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa Idara ya Habari (MAELEZO) kutoa fursa kwa Wakuu wa Mikoa kueleza mafanikio yaliyopatikana kwenye maeneo yao.
Amesema kuwa Mkoa wa Arusha umefanikiwa kutekeleza Mpango Mkakati wa upatikanaji wa huduma bora za afya kwa kuzingatia afya ya msingi kuwafikia wananchi katika maeneo yao kwa lengo la kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.
“Kati ya fedha hizo Bilioni 57.07 zimetumika kuboresha miundombinu ya afya ikiwemo ujenzi, ukarabati na ukamilishaji wa majengo na shilingi Bilioni 26 zimetumika katika manunuzi ya dawa, vifaa tiba na vitenganishi,” amesema Mhe.Kihongosi
Aidha amesema kuwa juhudi hizo za mafanikio zimeweza kuongeza idadi ya vituo vipya vya kutolea huduma za afya 87, kutoka Vituo 249 hadi vituo 350, sawa na asilimia 71.14 .
“Ujenzi wa Hospitali mpya 8 na kuufanya Mkoa kuwa na jumla ya Hospitali 21, zikiwa na majengo ya kutolea huduma za dharura (EMD),Ujenzi wa Vituo vipya vya afya 8, na kuufanya mkoa kuwa na Vituo 66 pamoja na Ujenzi wa Zahanati mpya 38, na kuufanya Mkoa kuwa na jumla ya Zahanati 350.”amesema
Hata hivyo amesema kuwa katika huduma za kibingwa mpya 11 zimeanzishwa ikiwemo,upasuaji, pua, koo na masikio, mifupa, magonjwa ya figo, magonjwa ya ngozi, uchunguzi wa magonjwa ya saratani, magonjwa ya uzazi na mtoto, magonjwa ya afya ya kisayansi, magonjwa ya ndani, watoto, mfumo wa mkojo.
Amesema kuwa hali ya upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitengenishi imeongezeka kufikia asilimia 93 (2025) kutoka asilimia 65 (2021)
“Mashine za kisasa zimesimikwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mount Meru, ikiwemo: CT-Scan, ECHO, ECG na MAMOGRAPHY. Uwepo wa mashine hizi umepunguza rufaa za wagonjwa kwenda Hospitali za Rufaa nje ya Mkoa, kama KCMC (Kilimanjaro) na Muhimbili (Dar es Salaam).”amesema
Pia amegusia sekta ya utalii ambapo amesema Mkoa wa Arusha umepokea Kiasi cha shilingi Bilioni 103 kwa ajili ya uboreshaji wa Viwanja vya Ndege viwili, Uwanja wa Ndege Arusha eneo la Kisongo na Uwanja wa Ndege ziwa Manyara, kiasi hicho cha fedha kimefanya maboresho ili kuvipa hadhi na kuongeza idadi ya abiria kufuatia idadi ya miruko.
Mkoa wa Arusha ni miongoni mwa Mikoa 31 nchini, wenye Wilaya sita, Halmashauri saba, Tarafa 23, Kata 158, Vijiji 394, Mitaa 154, na Vitongoji 1,505 wenye jumla ya wakazi 2,356,255, kulingana na Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022.
Kati ya watu hao wanaume ni 1,125,616 na wanawake ni 1,230,639, kukiwa na wastani wa ongezeko watu kwa asilimia 3.4% kwa mwaka.