Na WAF, Dodoma
Watumishi wa Wizara ya Afya wa Makao Makuu ya Wizara leo Julai 21, 2025 wamehamia rasmi na kuanza rasmi kutoa huduma kwa wananchi katika jengo jipya la Wizara ya Afya lililopo Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma.
Hatua hiyo inajiri mara baada ya kukamilika kwa jengo hilo ambalo limegharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 26.6 na sasa litawawezesha watumishi wote wa Wizara ya Afya makao makuu kufanya kazi katika eneo moja, na kuleta ufanisi na tija zaidi kwa huduma zinazotolewa.
Jengo hilo lina mita za mraba 14,355 likijumuisha sakafu 10 huku mbili(2) zikiwa ni sakafu za ardhini (basement), jengo lina ofisi zaidi ya 188 pamoja na kumbi za mikutano 13.
Wananchi wote wenye uhitaji wa kupata huduma wakaribishwa kufika katika ofisi hizo mpya muda wa saa za kazi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (07:30 am) mpaka saa tisa na nusu mchana (03:30 pm) Jumatatu mpaka Ijumaa.