Winga Offen Chikola, amesema kwake itakuwa rahisi kujitangaza na kupata soko la kucheza la kulipwa nje ya Tanzania baada ya kujiunga na Yanga.
Chikola anasema hata alipopigiwa simu kwa mara ya kwanza na Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said, kwake ilikuwa kama ndoto, kwani kwa uwezo wake alikuwa anatamani acheze kwenye klabu ambayo inaonekana zaidi kwenye michezo ya kimataifa kwa ajili ya kujitangaza zaidi.
“Hersi, aliongea kama utani hivi, unataka kuendelea kucheza kwenye klabu zako hizo za huko?, lakini ukweli hata mimi mwenyewe nilitamani kucheza klabu kubwa kwa sababu timu nyingine ningechelewa sana kuonekana,” anasema Chikola.