Klabu ya Simba imemalizana na kiungo wa Azam FC, Feisal Salum Abdallah, Simba wamependekeza kumpa Feisal mkataba wa miaka miwili pekee, ambapo atahudumu Simba SC kuanzia msimu wa 2025-2026 mpaka 2026-2027.
Feisal amewagomea waajiri wake Azam FC kuhusu kumsainisha mkataba mpya, chanzo changu kinasema “Feisal hataki kubaki Azam, Feisal anataka kucheza Simba tena anatamani akacheze Champions League” kilisema chanzo hicho.
Kilichobaki ni mazungumzo kati ya Azam FC na Simba SC yafanyike ili Fesal aweze kusaini Simba SC, narudia FEISAL HAITAKI AZAM