DAR ES SALAAM: KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Hemed Morocco, amesema kikosi chake kipo tayari kikamilifu kuanza mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN), huku akisisitiza kuwa wachezaji wake wako vizuri kiakili, kimbinu na kimwili.
Akizungumza na waandishi wa habari Morocco amesema maandalizi ya kikosi hicho yamekwenda vizuri, na sasa wanajiandaa kwa mchezo wa ufunguzi kwa ari na morali ya juu.
Stars inatarajia kucheza na Burkina Faso katika mchezo wa kwanza hatua ya makundi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jumamosi.
“Wachezaji wako tayari – kimchezo, kimbinu, kiakili na kisaikolojia. Tumejifunza kutoka mechi za maandalizi na sasa tuko tayari kupambana. Lengo letu ni kushambulia na kupata matokeo chanya,” amesema Morocco.
Ameongeza kuwa kikosi chake kimekuwa na mafunzo ya kina kwa siku kadhaa, wakijikita zaidi kwenye mbinu za kushambulia na kudhibiti kasi ya wapinzani.
The post Stars yaiva kwa CHAN first appeared on SpotiLEO.