NIGERIA: MTAYARISHAJI maarufu wa maudhui kutoka Nigeria, Chekwas Okorie, maarufu Gorilla Guy, kwa mara ya kwanza ameeleza kwa nini ameamua kutumia uhusika wa Gorilla badala ya mwanadamu wa kawaida katika uigizaji wake.
Chekwas, anasema aliamua kufanya hivyo kwa kuwa aliona fursa ya kupata fedha kupitia uhusika huo lakini pia kujenga wafuatiliaji wake kwa haraka jambo ambalo lilimbadilisha mno kimaisha.
Akiongea kwenye video iliyosambazwa kwenye mtandao wa Instagram, mtumbuizaji huyo amesema:
“Mambo ni magumu sana nchini Nigeria. Fanya chochote kinachohitajika ili kuishi, kisheria.
Niliacha kuwa mwanadamu mwaka 2023. Nilianza kuwa sokwe na katika miaka miwili tu, nimepata mara tano ya yote niliyofanikisha maisha yangu yote kama mwanadamu,” amesema.
“Siku hizi ukiniona hadharani ukiniita sokwe nakuita binadamu hata sijali, nilipokuwa binadamu nilifanikisha nini? Unakuwa unatengeneza umaarufu na kujulikana na wengi lakini mfukoni hakuna kitu lakini ubunifu nilioufanya unaniingizia pesa nyingi,” ameongeza.
The post Gorilla Guy: Usokwe unaniingizia pesa nyingi first appeared on SpotiLEO.