UONGOZI wa JKT Tanzania umebainisha kuwa wachezaji wao wote muhimu wana mipango nao hivyo itakuwa ngumu kwao kuondoka kwenda kupata changamoto mpya kwa msimu ujao.
Ilikuwa inaelezwa kuwa timu zenye maskani yake Kariakoo ikiwa ni Simba SC na Yanga SC zilikuwa zinawania saini ya beki wa JKT Tanzania huku Simba SC ikipiga hesabu kupata saini ya kipa wa JKT Tanzania.
Kwa maana hiyo kipa Yacoub Selemani na Wilson Nangu ambaye ni beki bado wapo ndani ya JKT Tanzania kuelekea msimu mpya wa 2025/26 baada ya madili yao kuzuiwa.
Nangu na Yacouba ambao wapo katika kambi ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inayoshiriki CHAN na Agosti 6 itakuwa na mchezo dhidi ya Mauritania, Uwanja wa Mkapa saa mbili usiku.
Ofisa Habari wa JKT Tanzania, Masau Bwire anasema kuwa “Nangu na Yacouba wapo na wataendelea kuwepo hadi hadi 2028, hatuna mpango wa kuwauza kwa sasa kutokana na malengo tuliyokuwa nayo msimu ujao.