DAR ES SALAAM:MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Abdul Idd ‘Lavalava’, ametambulisha EP yake ikiwa ni ya kwanza tangu kuachana na lebo yake ya zamani ya WCB chini ya Nassibu Abdul ‘Diamond platnumz’.
EP( Extended Playlist) hiyo inayoitwa TIME ina nyimbo tano akiwashirikisha wasanii Yasrun Shaban ‘Yammi’ kwenye wimbo wa Aste Aste, na Nicolas Lyimo ‘Billnass’ katika wimbo wa V.I.P. Nyimbo nyingine ni Kiss me, Ningefanyaje na Ngekewa.
Kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii, Lavalava ameachia kazi hizo na kuwashukuru wote waliomsaidia kufanikisha mradi huo.
“Hizi ndio nyimbo zetu, kiukweli nina furaha sana kutambulisha kwenu EP yetu ya Time. Niwashukuru watu wote nilioshirikiana nao kukamilisha hili, pia niseme tu nimewamiss sana mashabiki zangu,” amendika Lavalava.
EP hiyo inatarajiwa kuonesha upeo mpya wa ubunifu wa Lavalava na kutoa ladha tofauti kwa mashabiki wake, ambao wamekuwa wakisubiri kazi mpya kutoka kwake tangu alipoanza kujitegemea kimuziki.
The post Lavalava atambulisha EP yake first appeared on SpotiLEO.