Wote tunajua inapofika hatua ya mikwaju ya penati, ustadi wa golikipa ndio huamua mshindi wa mchezo.
Jambo hilo ndilo lililodhihirika juzi kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii nchini Uingereza ambapo akili na ustadi wa golikipa wa Crystal Palace Dean Henderson uliweza kuizawadia taji la Ngao ya Jamii Shield klabu yake iliposhinda dhidi ya Liverpool.
Henderson aling’ara kwa kuweka kwapani penati mbili muhimu, akitumia “karatasi maalum ya majina” iliyokuwa imebandikwa kwenye chupa yake ya maji, yenye maelezo ya wapi wachezaji wa Liverpool hupiga penati zao.
Taarifa zinaeleza kuwa Henderson alijiandaa mapema kabla ya mchezo, akitumia muda kusoma tabia za wapiga penati wa Liverpool. Mbinu hiyo ilimsaidia kutabiri upande ambao mpira ungeelekezwa, na mara mbili akaokoa kwa ustadi mkubwa.Henderson alipangua Penati ya Alexis Mac Allister pamoja na Harvey Elliot, huku ya Mo Salah ikipa juu yaa nguzo.
Baada ya mchezo huo akiwa na furaha tele, Henderson alimpatia shabiki mmoja wa Palace chupa hiyo yenye maelezo ya siri yaliyowapa ushindi.