Mshambuliaji mpya wa Simba Jonathan Sowah jana alifungia bao timu hiyo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Carabat FC.
Simba iko kambini nchini Misri kujiandaa na msimu mpya, jana ilicheza mchezo huo wa na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Bao lingine katika mchezo huo limewekwa kimiani na kiungo mpya mshambualiaji raia wa Kenya, Mohammed Bajaber.