Uongozi wa Klabu ya Young Africans (Yanga) umetolea ufafanuzi mchango wa Tsh. Milioni 100 uliotolewa kwa Chama Cha Mapinduzi (#CCM), Agosti 12, 2025, kuwa fedha hizo zilitolewa na Taasisi ya GSM Foundation, ambayo iko chini ya Ghalib Said Mohammed na si kutoka kwenye fedha za Wanachama au mapato ya klabu.
Kupitia taarifa yao, Uongozi wa #Yanga umeeleza ndani ya miaka mitatu GSM Foundation imekuwa ikishirikiana nao kutoa misaada kwa Jamii na makundi mbalimbali
Taarifa hiyo imeeleza kuwa klabu inaomba radhi wanachama wake kutokana na sintofahamu iliyotokana na mchango huo kwa CCM.