MSHAHARA wa kiungo wa Tanzania ambaye anacheza ndani ya kikosi cha Azam FC kinachotumia Uwanja wa Azam Complex kwa mechi za nyumbani unatajwa kuwa tishio kutokana na ukubwa wake na thamani ya kiungo huyo mzawa.
Ilikuwa inatajwa kuwa Yanga SC na Simba SC zilikuwa kwenye hesabu za kuwania saini ya kiungo huyo. Simba SC walikuwa wanapewa nafasi kubwa kuipata saini yake jambo ambalo limekwama mazima kutimia.
Taarifa zinaeleza kuwa Azam wamempa Feisal hela binafsi ya kusaini mkataba mpya (Sign on fee ya Tsh 800m cash). Mshahara wa Tsh 50m (take home), kwa mwezi hii ni baada ya makato na kodi. Ubalozi wa Azam Pesa ambapo kwa mwaka atalipwa Tsh 200m. Lakini pia Azam wame-activate kipengele cha mauzo yake ‘buyout clause’ yake kutoka $500,000 na sasa inatajwa ni $800,000.
Ikumbukwe kwamba Kocha Mkuu wa Azam FC, Florent Ibenge aliwambia viongozi wake wasimuuze Fei Toto ndani ya dirisha hili. Kocha huyo aliwambia wamzuie kiungo huyo kwa gharama yoyote kwani kikosi chake kipya kitajengwa kupitia Feisal.