Brighton inahitaji Pauni 100 milioni ili kumuuza kiungo wao wa kati Carlos Baleba, 21, baada ya Manchester United kuonyesha nia ya kumsajili.
Baleba, aliyesajiliwa kutoka Lille mwaka 2023, amekuwa mhimili muhimu wa safu ya kiungo ya Brighton msimu uliopita akicheza mechi 33, pia alishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa klabu hiyo.
Hata hivyo, Man United haina mpango wa kutoa kiasi hicho ingawa ofa yao ya kwanza inaweza kufikia Pauni 60 milioni.